Kivuko Na Watoto: Mafunzo yenye kuleta mabadiliko kwa watoto na walezi wao waliioathirika na VVU

Kivuko Na Watoto: Mafunzo yenye kuleta mabadiliko kwa watoto na walezi wao waliioathirika na VVU

by Gill Gordon
Kivuko Na Watoto: Mafunzo yenye kuleta mabadiliko kwa watoto na walezi wao waliioathirika na VVU

Kivuko Na Watoto: Mafunzo yenye kuleta mabadiliko kwa watoto na walezi wao waliioathirika na VVU

by Gill Gordon

Paperback

$39.95 
  • SHIP THIS ITEM
    Qualifies for Free Shipping
  • PICK UP IN STORE
    Check Availability at Nearby Stores

Related collections and offers


Overview

Kupata VVU inaweza isiwe hukumu ya kifo, lakini madhara yake bado ni makubwa. Watu wengi wanaoishi na VVU wanakabiliwa na ukanaji na kutokuwa na hakika kuhusu mustakabali wao, na wasiwasi huu unaweza kuonekana kwa undani zaidi kwa watoto na vijana. Kivuko na Watoto kinawapa mashirika na watu binafsi kitabu ambacho wanaweza kukitumia kuwahusisha watoto walioathirika kwa VVU na walezi wao, kwa kutumia mazoezi yenye uwezo mkubwa wa kuwasilisha taarifa, kuchunguza kanuni, kugundua uwezo wao, na kila mtu binafsi na kwa pamoja kuunda njia madhubuti za ustawi. Vipindi vya mafunzo vinajumuisha mada nyingi kwa kuzingatia mfumo wa haki za mtoto na jinsia ikiwa ni pamoja na ustawi wa kisaikolojia na kijamii na uimara, uthubutu, ukiwa, upimaji wa VVU, kuishi vizuri na VVU, kuzuia unyanyasaji wa kijinsia, na kuwasaidia walionusurika na unyanyasaji. Vinashughulika na masuala yanayowakabili vijana wanaokua, ambayo kwa hakika yanaweza kuwa na changamoto kwa wale walioathirika kwa VVU – kuanzia urafiki shuleni, hadi katika uhusiano, ujinsia, na njia za kujipatia riziki. Kila kipindi kati ya vipindi hivi kinaeleza kwa uwazi madhumuni yake makubwa, na kuweka lengo na njia kwa kila shughuli. Shughuli nyingi zinatekelezwa na washirikikwa kushirikiana na makundi rika yao matatu tofauti ya watoto wadogo (umri wa miaka 5-8), na watoto wakubwa (umri wa miaka 9-14) na walezi. Wakati mwinigine kila kundi rika hufanyakazi katika makundi madogo madogo ya jinsi. Makundi rika hayo wakati mwingine hufanya kazi pamoja, au kujumuika pamoja kushrikishana walichojifunza na kujadili njia zingine za kuhusiana. NOTE not for sale from this publisher in Uganda and Tanzania

Product Details

ISBN-13: 9781853399138
Publisher: Practical Action Publishing
Publication date: 07/31/2016
Pages: 472
Product dimensions: 6.25(w) x 9.75(h) x (d)

About the Author

Gill Gordon

What People are Saying About This

From the Publisher

UKIMWI unahusu haki ya kijamii. Hatuwezi kufikia malengo yetu ya kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030 mpaka tutimize mahitaji ya jamii nyingi zinazoishi katika mazingira magumu, mara nyingi watoto na vijana wanaoishi na VVU na wanaoathiriwa na virusi. Kivuko na Watoto inatoa njia ambayo jamii zinaweza kusaidia na kulea watoto hawa na kujenga uthabiti wao. Hili ndilo ambalo ni lazima tulifanye kwanza – kuwajali wanaoishi katika mazingira magumu. Michel Sidibe, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS ‘Huu ni mwongozo muhimu sana kwa watoto na walezi. Mwongozo huu utasaidia kujenga uhusiano wa karibu zaidi kwa kutumia mawasiliano yenye maana/muhimu yanayosaidia watoto na walezi kukabili vikwazo na kujenga kaya iliyofungamana na kusaidiana.’ Martha Tholanah, Mwenyekiti wa Kimataifa, International Community of Women Living with HIV/AIDS ‘Natamani kuwa watoto wote wenye umri wa miaka 5 – 14 na walezi wao walioathiriwa na VVU wangepata fursa ya kufurahia Kuvuko na Watoto. Ninaamini kwamba kitawasaidia kutimiza ndoto zao na kushinda changamoto zao. Ni mwongozo wa kipekee kwa sababu unashughulika na makundirika peke yao na kwa pamoja na kushughulikia masuala mengi – ya kisaikolojia, kimwili, kijinsia, kiyakinifu na kiroho – yenye umuhimu mkubwa kwetu sisi sote’ Vincent Mwale, Waziri wa Vijana na Watoto, Zambia ‘Programu na miongozo kama Kivuko na Watoto vinaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa binadamu kati ya maendeleo bora na dira ya dunia yenye uwezekano, na katika matukio ya upeo wa juu, maisha yaliyozingirwa na kifo.’ L'Orangelis Thomas, mwanamke kijana anayeishi na VVU ‘Gill Gordon hana budi kupongezwa kwa kuandika mwongozo unaovutia kusoma na kutumika. Kivuko na Watoto kimejaa vidokezo halisi vya namna ya kutenda, na muhimu zaidi kina hazina/mkusanyiko wa kutosha wa mazoezi kwa vitendo. Kitabu hiki kitakuwa marejeo yanayofaa zaidi kwa daktari yeyote anayewashughulikia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na vijana.’ Morten Skovdal, Profesa Mshiriki, Department of Public Health, Universityof Copenhagen ‘Inafurahisha sana kuona upeo wa fikra muhimu na vitendo katika kushughulikia watoto walioathiriwa na VVU. Marejeo haya yanatoa programu bora ya mafunzo inayotokana na mafanikio makubwa ya Kivuko na Watoto. Iwapo tutakipa muda wa kutosha na nia thabiti kwa mbinu yake ya kufundishia, Kivuko na Watoto kina uwezo mkubwa wa kushughulikia upungufu muhimu katika mwitikio wetu kwa watoto walioathiriwa na VVU .’ Kate Iorpenda, Mshauri Mwandamizi, Watoto na Vijana Balehe, International HIV/AIDS Alliance ‘Mwanzoni wakati PASADA ilipoanza kutumia Kivuko, watu walidhani shirika hilo lina wazimu. Baadaye walitambua kuwa kilikuwa ni nyenzo muhimu na yenye uwezo mkubwa kwa jamii. Laiti sauti yangu ingeweza kusikika duniani kote ningewaambia watu watumie Kivuko na Watoto kwa sababu kitabadili maisha yao na namna wanavyojifikiria kuhusu VVU na UKIMWI.’ Mrisho Mpoto, Mshairi, Mwigizaji na Mwanamuziki ‘Gill Gordon ana kipaji kikubwa cha kuandika miongozo inayochochea kujitambua na wakati huo huo kujenga kujiamini, kuthubutu, na stadi nyingi muhimu za maisha. Analeta utajiri wake mkubwa wa uzoefu wa kufanyakazi pamoja na vijana katika masuala mengi tofauti. Bila ya shaka, nitayatumia mawazo haya na kuyatohoa kwa ajili ya watoto wadogo katika miktadha mingine.’ Ross Kidd, Participatory Mkufunzi Shirikishi na Mwandishi wa miongozo mbalimbali, ikiwemo Kuelewa na Kukabili VVU ‘Tunapenddekeza kwa dhati, Kivuko na Watoto kuwa kitabu pekee katika kusaidia utekelezaji wa ujinsia na afya afya ya uzazi na VVU na UKIMWI kwa Watoto.’ Zikhalo Phiri, Mtendaji Mkuu wa Young, Happy, Healthy and Safe, Zambia

From the B&N Reads Blog

Customer Reviews